Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 19, 2012

AJALI YA MELI YA SKAGIT PICHANI VIWANJA VYA MAISALA

Wananchi Wakiwa katika Viwanja vya Maisara Kutambua Miili ya Jamaa Zao.

Watalii kutoka Nchini Italia wakiwa katika viwanja vya maisara katika zoezi la klutambua miili ya Watu waliofariki kastika ajali ya boto ambayo walikuwemo Watalii na kati yao mmoja amefariki katika ajali hiyo.

Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya maisara ili kutowa pole kwa Wananchi waliofiwa na jamaa zao.
Rais Mstaaf  Mhe Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika eneo hilo maalum kwa ajili ya kuwatambua maiti wa ajali ya boti.
Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Dk. Marijani , alipofika katika viwanja vya maisara kutowa pole na kuangalia utaratibu wa kuwatambua marehemu na jamaa zao.



Jamaa  wa Marehemu Sauda Juma ambaye ni Raia wa Ruwanda ambaye ambaye amafariki katika ajali hiyo, wakisubiri maiti yao ili kwenda kuzikwa.
Mkurugenzi Biashara wa Kampuni ya Zantel  Zanzibar Mohammed Mussa,akikabidhi  msaada wa sada Katibu Mtendaji wa Wakfu Abdalla Talib,kwa  maiti wa ajali ya boti, makabidhiano hayo yamefanyika viwanja vya maisara,
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wakitowa huduma ya maji na biskuti kwa Wananchi wanaofika kutambua miili ya jamaa zao na watoa huduma katika kituo hicho.
Mmoja wa Abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Tatu Piela , akipata  kikombe cha uji kutoka kwa wasamaria waliofika katika viwanja vya maisara , ambaye na mweji wa Isaka Shinyanga, amepoteza  mtoto Said Jumanne mwenye umri wa miezi 9 wake, akisubiri kukabidhiwa maiyi yake kwa ajili ya kwenda kuzika.  

Waheshimiwa Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mashehe wakiwa katika viwanja vya maisara kuwafariji jamaana ndugu waliofiwa na jamaa zao.
Maofisa wa  Wakfu na Maali ya wakiandaa sanda kwa ajili ya kutowa kwa jamaa wa marehemu ili kuzikia  iliotolewa na Serekali kwa Wananchi waliofariki katika ajali hiyo. na kusaliwa katika viwanja hivyo.  

Maofisa wa Ubalozi wa  Scandinavia wakiwa katika viwanja vya maisara kukagua mwili wa mmoja wa Mtalii aliofariki katika ajali hiyo.
Wananchi  wakikagua maiti ili kutambua maiti za jamaa zao katika viwanja vya maisara ambavyo vimetengwa kwa ajili kufikisha maiti wanaookolewa katika ajali hiyo.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Asha Bakari Makame, akizungumza na waandishi wa habari  alipofika katika viwanja  vya maisara  alipofika kutoa pole kwa wananchi waliofiwa na jamaa zao.  
Meneja wa Kitengo cha Data  katika Wizara ya Afya Zanzibar Mohammed Habibu, akitowa idadi ya wananchi waliopokelewa na  majeruhi na wale waliofariki, kutokana na ajali hiyo, akiwa katika kituo cha kupokelea maiti maisara.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika viwanja vya maisara kulikotengwa kwa ajili ya kuwatambua marehemu wa ajali ya boti iliotokea jana 18-7-2012 katika bahari ya Zanzibar maeneo ya Chumbe,
Naibu Amir, Azan Hamdani, akizungumza na waandisahi wa habari katika viwanja vya maisara.
 Jamaa wa mmoja wa marehemu wa ajali ya Boti akiwa na simazi ya kuondokewa na jamaa yake katika tukio la ajali hiyo, baada ya kuitambua maiti ya jamaa yake iliopelekwa katika viwanja vya maisara.
 Baadhi ya Wanandugu wakiwa katika foleni kusubiri kutambua miili ya Ndugu zao waliopata ajali ya kuzama kwa boti ya Kampuni ya SeaGull.jana katika  bahari ya Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya mpira Mairasa kusubiri kutambua miili ya jamaa zao.

Wananchi wakiwa katika Ufukwe wa bahari ya Kizingo wakiangalia  kama kutakuwa na miili kuangukia katika ufukwe huo ili kuwatambua jamaa zao

TAARIFA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE 18 JULAI, 2012, CHUMBE, ZANZIBAR

Jana tarehe 18 Julai, 2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.

Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na Polisi waanze kazi ya uokoaji mara moja.

Habari kutoka blog ya:http://othmanmapara.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment