Pages

Ads 468x60px

Monday, October 22, 2012

SHANGWE SURPRISE KTK PARTY YA ANDREW CHALE

TIGO, AMERICAN GARDEN WA-SURPRISE WATOTO KATIKA 'HAPPY BIRTHDAY' YA ANDREW CHALE...!!!

 Birthday cake hiyooo
 Birthday boy akikata cake
 Wenceslaus Kisarika ambae ni Marketing Manager wa K&K pamoja  Cons  Ltd, akifungua shampeni ...Andrew Chale pembeni
Mtoto Mashaka Juma wa kituo cha Mitindo House, akimlisha keki kwa niaba ya watoto wenzake zaidi ya 50 waliojitokeza wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwandishi wa gazeti hili Andrew Chale,  jana iliyofanyika ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Tigo Tanzania na American Garden
 Andrew Chale akiwa katika picha ya pamoja na watoto aliosherekea nao Birthday yake
KAMPUNI ya Tigo Tanzania Oktoba 21, imeweza kufanya ‘surprise’ mbalimbali kwa watoto waliojitokeza katika siku maalum ya kuzaliwa kwa mdau na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima na blog, Andrew Chale, iliyofanyika ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Katika party hiyo maalum, Andrew Chale amesema ni ya kwanza kabisa kwa Mtanzania kufanya hivyo kwani ilianza tokea  Oktoba Mosi  kwa kutembelea vituo vya watoto waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi  na kutoa misaada na pia kutembelea watoto mahospitalinio na kuwafariji.
Akielezea mtandao huu, Andrew Chale anasema alimwamini Mungu muda wote ndio maana ameweza kufika hapo na pia kutumia nafasi hiyo kwa pamoja kufurahi na watoto hao wakiwemo wale waishio kwenye mazingira magumu.
“Leo, ni siku muhimu sana kwangu, najiona nipo na mamilioni ya marafiki kwa kufika kwenu kumenitia sana faraja Mungu awabariki nyote” alisema Andrew  wakati akiwashukuru watoto mbalimbali waliojitokeza kufanya nao sherehe hiyo.
Watoto hao wakiwemo waliotoka kwenye vituo vya kulelea watoto vikiwemo vya  Tanzania Mitindo House kilicho chini ya Mbunifu,Khadija Mwanamboka, New Life Orphanage center  cha Kigogo, watoto waishio mitahani na wale wa majumbani walijumuika kwa pamoja na kufurahia na ‘Uncle’ wao Andrew Chale  ikiwemo kutembelea sehemu kadhaa za ndani ya jumba hilo la kumbukumbu na kujionea mambo mbalimbali.
Furaha hiyo ya siku maalum ya kuzaliwa kwa Andrew Chale imeweza kuongezwa utamu na kampuni ya Mawasiliano ya mtandao wa simu nchin, Tigo Tanzania, ambayo iliwezesha kumpatia keki na shampeni  maalum pamoja na zawadi zingine nyingi kwa watoto.
Kwa upande wake Ofisa wa masoko wa tigo, Benny  Lutaba, alipongeza kwa sherehe hiyo na kuomba jamii kuendelea kuwaunga mkono kwa bidhaa zao hapa nchini sambamba na kusaidia jamii kwa rika zote.
Nae Wenceslaus Kisarika ambae ni Marketing Manager wa K&K pamoja  Cons  Ltd  alipongeza kwa hatua ya watu kukumbuka watoto hasa waishio kwenye mazingira hatarishi na magumu hapa nchini.
“Tumefarijika sana kuunga kwenye siku hii muhimu, hakika jamii iiige mfano huu wa kuwakumbuka watoto hasa wanaohitaji msaada si utoe fedha hata kuwaleta mahala kama hapa ni moja ya kuwatimizia mahitaji yao” alisema Wence.
Aidham mbali na tigo,  American Garden kwa upande wao waliweza kuwa ‘surprise’ watoto  kwa kuwapatia zawadi za bidhaa zao zinazopatikana nchini kote.
Akizungumza na mtandao huu kwenye sherehe hiyo, Ofisa masoko wa Kingsway International (T) ltd,  American Garden, Miraji Chambuso  alipongeza kwa hatua hiyo ya kuwakumbuka watoto hao na ni moja ya kuhamasisha utalii wa ndani.
“Watoto wanapopata nafasi ya kufika sehemu kama hizi ni kuhasisha utalii wa ndani na sisi tupo mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto na malengo yao” alisema Miraji..
 

Sunday, October 14, 2012

       AR in A-TOWN! stay tuned for more details...
JAMBO FASHION NIGHT...

Friday, October 12, 2012


     WELCOME TO ARUSHA TRAVEL LODGE. FOR BOOKINGS CALL 0712357987

              ARUSHA TRAVEL LODGE  hotel  is located at the base of Mt. Meru, with an incredible view of   the majestic mountain. The brand new hotel is a touch of luxury on the outskirts of Arusha. Each room has the highest quality beds and linens, private bathroom, free WiFi Internet Access, flat screen television with cable channels, writing desk, wardrobe, mini fridge, and safe. Transportation is also available to and from the airport, city center, or all of the national parks like Serengeti or Ngorongoro!
                                    The Hotel view from outside...
                                                       The entrance.....
                                            The bedroom...

                                                        The big big bathroom....
You can even work from your bedroom and enjoy watching telly on a flat screen Tv

FOR BOOKINGS CALL: +255 712 357 987
EMAIL: info@arushatravellodge.com
WEBSITE: www.arushatravellodge.com

ARUSHA TRAVEL LODGE IS LOCATED IN NJIRO MAKABURINI. ARUSHA.TANZANIA.

YOUR ALL WELCOME TO STAY WITH US! AND FEEL AT HOME!!!

Wednesday, August 22, 2012



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UHAMASISHAJI WA KUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO, BONDE  LA NGORONGORO NA TUKIO LA KUHAMA WANYAMA KATIKA HIFADHI YA SERENGETI KATIKA SHINDANO LA MAAJABU SABA YA ASILI KATIKA BARA LA AFRIKA

Hiv karibuni  pamekuwa na  shindano  jipya  lijulikanalkama  Seven Natural   Wonders,                   linaloshindanisha vivutio     mbalimbali         vya         asili vinavyopatikana  katika  kila bara.  Shindano  hillinaloendeshwa  kwa kupiga      kura                   kupitia   tovuti ya                   http://sevennaturalwonders.org linashindanisha  vivutivya  utalii  kumi  na viwil (12) katika  bara la Afrika. Tanzania ni nchi pekee  yenyvivutio vingi katika orodha hiyo. Vivutio vya Tanzania ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi     ya                  Serengeti.   Watanzania     na       watu          wote                 duniani wanahamasishwa kuvipigia kura vivutio hivyo vitatu (3).

Ili  kurahisisha  upigaji  kura  kwa  vivutivya  Tanzania,  Bodi ya  Utalii Tanzania           imewaomba           waandaji wa    shindano   hilo     kuandaa         tovuti maalum             ambayo              ni    http://sevennaturalwonders.org/tanzania/ itakayomuhitaj mpigakura   kutum baru pep yeny kichwa  cha habari TANZANIA inayoorodhesha vivutio hivyo vitatu (3), na vivutio vingine  visivyozidi  vinne  (4)  vilivyopo Tanzania  ambavympigakura anaona vinafaa  viwemo  katika  orodha ya maajabsaba  ya asili  ya Tanzania,  kwenda kwenye anuani  hii  vote@sevennaturalwonders.org. Kwa            maelezo         zaidi      kuhusu           vivutio             vya    utalii              Tanzania tembelea www.tanzaniatourism.go.tz.

Shindano     hili linaweza  kuwa fursa nzuri  kwa Tanzania  kujitambulisha pamoja na kuitangazia dunia kuwa Mlima Kilimanjaro, ambao  ni mlima mrefu kuliko yote barani  Afrika;  Hifadhi ya Serengeti,  ambapo tukio  la kuhama  wanyama  hutokea  kila  mwaka;   na  eneo  l Ngorongoro, ambalo ni urithi wa dunia wa asili na utamaduni (natural and cultural World Heritage Site), vyote ni vivutio vilivyopo hapa kwetu Tanzania.

Vivutio    vitakavyoshinda     vitatangazwa     na     vyombo     mbalimbali     vya habari duniani na kupewa hadhi zaidi ya kimataifa.

Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vyote vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika.

Imetolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji
BODI YA UTALII TANZANIA