Pages

Ads 468x60px

Monday, June 18, 2012

Jim Iyke:Natoa 5% ya maisha yangu kujikingana skendo

STAR WA NOLLYWOOD WIKI HII
                           Jim Iyke
Jim Iyke:
Natoa asilimia 50 ya maisha kujikinga na skendo

LAGOS, NIGERIA
KATIKA makala hii tutaangalia mahojiano yaliyofanywa kati ya mwigizaji, Jim Ike na televisheni moja maarufu ya jijini hapa akielezea maisha yake kwa ujumla na namna anavyojikinga na skendo kama zinavyowakuta nyota wengine wa filamu nchini Nigeria.

TV: Tunaomba kujua jina lako ulilopewa na wazazi wako?
IYKE: Vizuri, jina langu ni James ambalo nafupisha na kuita Jim, na Ikechukwu nikifupisha kwa kuita Iyke ambalo lilitumiwa na babu aliyekuwa wa kabila ya Ibo likimaanisha ‘nipo tofauti na wapumzikaji’.

TV: Ulianza vipi hadi kuwa hivyo ulivyo?
IYKE: Sikuwahi kufikiria kuwa mwigizaji hapo kabla katika makuzi yangu, ila ndoto hiyo ilianza kuibuka baada ya kumaliza shule miaka 12 iliyopita, wakati huo nilikuwa nikifanya kazi benki, ndipo nilianza kwa kuandika hadithi ya filamu, lakini baada ya kuimaliza rafiki zangu walinishauri na mimi kuigiza pia, hapo ikawa mwisho wangu wa kuhesabu fedha za watu. Hapo nikawa mwandishi na mwigizaji.

TV: Ni faida ipi uliyoipata kupitia sanaa?
IYKE: Faida kubwa niliyoipata kwanza ni kujitegemea kwa kuwa na kwangu, na kuhama kwenye nyumba ya wazazi wangu. Nimekuwa nikiandaa matamasha ya burudani na matukio tofauti ambayo yamekuwa yakiniingizia fedha. Ukiachilia filamu, pia huwa najihusisha na masuala ya mitindo katika kampuni yangu na nimekuwa nikivaa nguo zenye chata ya ‘showbiz’.

TV: Unawezaje kujikinga na usumbufu wa wanawake kama mtu maarufu? 
IYKE: Maisha yangu nimeyatoa kafara kwa watu wengine kwa sababu maisha yangu ya kawaida yanafuatiliwa na watu wa kawaida, kwani nimekuwa nikitoa asilimia 50 ya maisha yangu kwa ajili ya kujikinga na habari za skendo zitakazozalishwa na watu wasiopenda maendeleo yangu.
Kwa kuhakikisha hayo yanatimia, nimekuwa nikitumia gari lililozibwa kwa vioo vyeusi na huwa siingii klabu au kwenye matukio ya muziki yanayohusisha watu wengi.

TV: Yapi matokeo yanayotokana na kuigiza maeneo ya mahusiano?
IYKE: Nimepata matatizo mengi hasa kwa kupitia mtandaoni, ambako nimekuwa nikitumiwa SMS zaidi ya 100 kwa kila siku kutoka kwa wanawake.

TV: Unazungumziaje maendeleo ya tasnia ya filamu mjini hapa?
IYKE: Biashara ya filamu imeshuka sana, hivyo nimekuwa nikijihusisha na biashara nyingine hali inayonisaidia kuongeza kipato zaidi nikiwa naongoza biashara za familia.

TV: Kwa sasa una umri gani?
IYKE: Nina umri wa miaka 34.

TV: Ukiwa ulitambulishwa na filamu ya ‘Between Kings and Queens’ ni vipi ulijipatia uzoefu?
IYKE: Ninaipenda filamu hiyo kwa sababu ilinitambulisha na nilitumia Uafrika wangu kupata uzoefu wa kuiigiza.

TV: Vipi unayo kampuni ya filamu?
IYKE: Ninayo kampuni yangu ya filamu inayojulikana kama Untamed Productions, na nimeshatengeneza filamu nyingi na baadhi yake ni ‘Two Dollars’, ‘Shades of White’ na nyingine.

TV: Ukiachilia tasnia ya filamu, ni kazi gani nyingine unajishughulisha nayo ya kusaidia jamii ya mjini hapa?
IYKE: Nimekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu… nimefungua mfuko wangu wa kujishughulisha na kazi hiyo.
Kwa kupitia mfuko huo zaidi ya vijana 8,000 wa Abuja wamesaidiwa.
Ukiachilia mfuko huo wa msaada, huwa najihusisha na kutangaza kipindi cha televisheni cha mazungumzo kinachojulikana kama ‘Jewel for Jim’. Kipindi hicho mara nyingi kimekuwa kikihamasisha uchangiaji wa mfuko huo.

TV: Tulipata habari za wewe kujishughulisha na masuala ya muziki.
IYKE: Kweli nimekuwa nikijishughulisha na muziki, ingawa mimi si mwimbaji. Lakini nimefungua studio ambazo ni maalum kwa ajili ya kusaidia vijana wenye vipaji na hawana uwezo wa kuingia studio.

TV: Mpaka sasa umeshaanza na vijana wangapi?
IYKE: Wengi, lakini bado nina mipango ya kuwasainisha zaidi walio na vipaji na hawana uwezo wa kutengeneza kazi.

0 comments:

Post a Comment