Marioa Van Peebles akiwa na wadau kwenye viwanja vya MAMBO CLUB vilivyopo ndani ya Ngome kongwe, akiwa sambamba na mwanae, Mandela na meneja wake, (kulia). |
Na Andrew Chale, Zanzibar
MWANDAAJI,Mtunzi na muigizaji wa filamu nyota wa Hollywood kutoka Amerika, Mario Van Peebles `MVP', amesema yupo tayari kufanya filamu Tanzania hususani Visiwa vya Zanzibar kutokana na maeneo mengi kuvutia kwa ajili ya filamu.
Mario ambaye alitamba na filamu mbalimbali ikiwemo ya Solo, iliyopata umaarufu mkubwa, alisema hayo visiwani hapa mjini Unguja muda mfupi wa kuzindua filamu ya ‘We The Party’ ndani ya ukumbi wa Ngomekongwe, linapoendelea tamasha la filamu za nchi za majahazi maalufu ZIFF 2012,msimu wa 15, ambayo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi kwenye skilini kubwa ambapo ndani ya filamu hiyo kinara wake ni Mtoto wake, ajulikanae Mandela Van Peebles.
Ambapo alisema kuwa, Zanzibar imebarikiwa kuwa na maeneo mengi mazuri na ya kuvutia ambapo endapo atachukua uamuzi wa haraka haraka ataweza kuja kucheza filamu yake ambayo itashangaza ulimwengu. “Nimevutiwa na Zanzibar na ...kwa juu ya kufanya jambo ni kuja siku moja kuigiza filamu nzuri hasa kulingana na maeneo yake na hakika itaweza kuvutia wengi duniani” alisema Mario.
Mario pia aliwataka watunzi wa filamu bara la Afrika kuchukua hatua na kutunga filamu za ubora na wao waje kujulikana zaidi kama ilivyo kwa waigizaji wa nchi za Ulaya, Amerika,India na falme za kiarabuambao wameendelea na kuwa na makampuni ya makubwa ikiwemo Hollyhood,Bollwood na nyingine nyingi.
Aidha, kwa upande wake, Mandela alisema kuwa alifurahia kufuata nyayo za baba yake katika sanaa ya uigizaji na kusema kuwa ameweza kutimiza ndoto yake na huo ni mwanzo na anataka kuja kuwa bora zaidi kama ilivyo kwa baba yake mzazi
Katika filamu hiyo, Mandela ameweza kuonyesha kiwango kikubwa cha ugizaji sambamba na wasanii wakubwa akiwemo Snop Dog Dog na Mario mwenyewe.
Filamu hiyo ya 'wE The Party' ndio kwa mara ya kwanza imezinduliwa barani afrika kwenye tamasha la filamu za nchi za majahazi zanzibarm (Zanzibar International Filamu Festival-ZIFF 2012) Aidha Mkurugenzi mkuu wa ZIFF, Profesa Ikaweba Buting alisema kuwa ni fursa ya pekee kwa tukio hilo na linaingia kwenye kumbukumbu ya ZIFF.
Miongoni mwa filamu zngine alizocheza ni New Jack City', Solo, ‘Exterminator’, ‘Full Eclipse’ ‘All things Fall Apart’ na nyingine nyingi.
Tamasha hilo lililodhaminiwa na ZUKU kwa miaka 10, filamu mbalimbali zinaonyeshwa sambamba na kutolewa na mafunzo ya kuandaa na kuongoza filamu kutoka kwa wandaaji maarufu duNIANI.
0 comments:
Post a Comment