Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 10, 2012

Tamasha la ZIFF lafunguliwa rasmi
    Miongoni mwa waanzilishi wa ZIFF hapa Tanzania, Farouque Abdallah-MC wa ufunguzi huo
    Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ali Khalil Mirza, akihutubia wageni mbalimbali akiwa kama Mgeni rasmi.
     Mkurugenzi mkuu wa ZIFF, Profesa Ikaweba Bunting
     Mwenyekiti wa Wananchi Group, Ali Mufuruki 




Na Andrew Chale, Zanzibar


TAMASHA la 15 la kimataifa la filamu za Nchi za Majahazi ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka (ZIFF) usiku wa Julai 7.2012, lilizinduliwa rasmi kwa shamrashamra mbalimbali ndani ya viunga vya Ngome Kongwe Mjini Unguja.

Akiongea mbele ya umati wa wageni kutoka ndani na nje ya Zanzibar waliofika kushuhudia ufunguzi huo wa tamasha hilo, Mkurugenzi mkuu wa ZIFF, Profesa Ikaweba Bunting, aliwashukuru kwa kuwaunga mkono kila mwaka tangu kuanzishwa kwa tamasha la kwanza mpaka leo ambapo ni miaka 15.

Pia aliishukuru kampuni ya Wananchi Group, inayomiliki ving’amuzi vya ZUKU ambao wamedhamini tamsha hilo kwa dola za Kimarekani milioni moja kwa muda wa miaka 10.

Tamasha hilo lilifunguliwa na mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ali Khalil Mirza ambaye alilipongeza tamasha hilo kwa ukomavu wake visiwani Zanzibar na kuchangia pato kubwa la ongezeko la utalii na wageni mbalimbali wakati wa msimu.

“Tunawashukuru Wazanzibari na wageni wote kwa kuwa nasi bega kwa bega kila mwaka katika tamasha hili ambalo limekuwa chachu kubwa ya maendeleo na mambo mbalimbali katika msimu huu wa tamasha hivyo tunajisikia faraja kwa kuungwa mkono,” alisema Ikaweba.

Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa ZIFF, Mohmoud Thabit Kombo aliwashukuru ZUKU kwa udhamini wao huo huku akitoa fursa kwa kampuni nyingine kujitokeza kudhamini ili kufikia malengo zaidi ambayo yanafanywa kila mwaka na tamasha.

ZIFF litaendelea mpaka Julai 15 huku kila siku filamu mbalimbali zitaonyeshwa kwenye big screen za Ngome Kongwe sambamba na semina za mafunzo ya uandaaji na uongozaji wa filamu yatakayotolewa na waongozaji wakubwa kutoka Amerika, akiwemo nyota wa filamu ya Solo, New Jack City na America’s Most Wanted, Mario Van Peebles.

(Habari kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima-) 

0 comments:

Post a Comment