Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 22, 2012



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UHAMASISHAJI WA KUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO, BONDE  LA NGORONGORO NA TUKIO LA KUHAMA WANYAMA KATIKA HIFADHI YA SERENGETI KATIKA SHINDANO LA MAAJABU SABA YA ASILI KATIKA BARA LA AFRIKA

Hiv karibuni  pamekuwa na  shindano  jipya  lijulikanalkama  Seven Natural   Wonders,                   linaloshindanisha vivutio     mbalimbali         vya         asili vinavyopatikana  katika  kila bara.  Shindano  hillinaloendeshwa  kwa kupiga      kura                   kupitia   tovuti ya                   http://sevennaturalwonders.org linashindanisha  vivutivya  utalii  kumi  na viwil (12) katika  bara la Afrika. Tanzania ni nchi pekee  yenyvivutio vingi katika orodha hiyo. Vivutio vya Tanzania ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi     ya                  Serengeti.   Watanzania     na       watu          wote                 duniani wanahamasishwa kuvipigia kura vivutio hivyo vitatu (3).

Ili  kurahisisha  upigaji  kura  kwa  vivutivya  Tanzania,  Bodi ya  Utalii Tanzania           imewaomba           waandaji wa    shindano   hilo     kuandaa         tovuti maalum             ambayo              ni    http://sevennaturalwonders.org/tanzania/ itakayomuhitaj mpigakura   kutum baru pep yeny kichwa  cha habari TANZANIA inayoorodhesha vivutio hivyo vitatu (3), na vivutio vingine  visivyozidi  vinne  (4)  vilivyopo Tanzania  ambavympigakura anaona vinafaa  viwemo  katika  orodha ya maajabsaba  ya asili  ya Tanzania,  kwenda kwenye anuani  hii  vote@sevennaturalwonders.org. Kwa            maelezo         zaidi      kuhusu           vivutio             vya    utalii              Tanzania tembelea www.tanzaniatourism.go.tz.

Shindano     hili linaweza  kuwa fursa nzuri  kwa Tanzania  kujitambulisha pamoja na kuitangazia dunia kuwa Mlima Kilimanjaro, ambao  ni mlima mrefu kuliko yote barani  Afrika;  Hifadhi ya Serengeti,  ambapo tukio  la kuhama  wanyama  hutokea  kila  mwaka;   na  eneo  l Ngorongoro, ambalo ni urithi wa dunia wa asili na utamaduni (natural and cultural World Heritage Site), vyote ni vivutio vilivyopo hapa kwetu Tanzania.

Vivutio    vitakavyoshinda     vitatangazwa     na     vyombo     mbalimbali     vya habari duniani na kupewa hadhi zaidi ya kimataifa.

Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vyote vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika.

Imetolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji
BODI YA UTALII TANZANIA