Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 2, 2012

WAZEE WASTAAFU WAMTAKA PINDA KUSIKILIZAMADAI YAO



Mzee Mafita (kulia) akiwa na boga leke( kushoto) ni Andrew Chale,Mkurugenzi wa Habarimotomototz  Inc.
Mzee Mafita na wenzake zaidi ya 8,000 ambao ni wastaafu wanadai mkuongezewa Pensheni zao kutoka elf 50, na pia wapewe penshi hizo kwa wakati.

Na Blogger team

WAZEE wastaafu  Serikalini wamemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusikiliza kilio chao cha muda mrefu ikiwemo cha kuwaongezea pensheni zao na kuwapatia kwa wakati.

Akizungumza  mapema leo jijini Dar es Salaam, mmoja wa wazee hao James Mafita Mkazi wa Dar es Saalam, ambaye alikua mfanyakazi wa wizara ya kazi na ustawi wa jamii wakati huo, alisema kuwa zaidi ya wazee 8,000 ambao wanapata pensheni kutoka wizara ya Fedha, wamekua wakicheleweshewa kuingizwa fedha hizo licha ya kua ni kidogo.

“Mwaka, juzi, wakati wa kilele cha siku ya wazee Duniani, Oktoba Mosi, tuliweza muomba waziri mkuu atuongezee pensheni na tupate kwa wakati, lakini tunaona kimya maana kiasi cha 50,000 kwa wazee ambao hatuna kazi ni unyonyaji” alisema Mafita.

Mafita aliongeza kuwa licha  ya kuendelea kuomba ongezeko lao hilo la pensheni kwa Waziri mkuu, waliweza kuwakilisha tena kwenye kilele cha wazee mwaka jana iliyofanyika Mkoani, Lindi lakini bado hawajasilikilizwa.

“Sie wazee tumewezesha nchi hii kwa kuitumikia, lakini wameshindwa kutujali wengine tunafanya kazi kuuza maboga mitaani, lakini wao wanajipatia malupulupu umengi na kushindwa kutukumbuka” alisema Madita.

Mbali na hilo, aliomba wazira ya Fedha kuwapatia pensheni zao hizo kwa wakati kwani utaratibu uliopo sasa wanawacheleweshea kwa kuwapatia zaidi ya miezi minne tofauti na awali walikua wakiwapa kwa wakati na kumtaka Pinda asikie kilio chao haraka kabla ya kuanza utaratibu mwingine kama wafanyavyo wazee wanaodai haki zao hapa nchini.

0 comments:

Post a Comment