Pages

Ads 468x60px

Friday, August 17, 2012


MBOWE,SUGU KUZINDUA TAWI JIPYA LA CHADEMA HOUSTON TEXAS MAREKANI

Tunapenda kutoa habari hizi kwa waTanzania wote na wapenda maendeleo, Siku ya Jumamosi Aug 25 kutakuwa na ufunguzi rasmi wa tawi la chama cha demokrasia na maendeleo Wageni rasmi wa ufunguzi wa tawi hilo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Jodeph Mbilinyi (Mr. 2/Sugu) Sherehe za ufunguzi wa tawi hilo zitaanza mida ya saa 

Saturday, August 11, 2012

REHMTULA KUJA NA “ALLY REHMTULLAH 2013 COLLECTION”

Rehmtullah katika pozi 

Rehmtullah katika pozi 

Rehmtullah katika pozi 



... kuzindua mitindo mipya  Serena Hotel, Septemba 8.

                                Na Andrew Chale(blogger team)
Mwanamitindo maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah ameandaa onyesho kubwa na la kipekee la mitindo hapa nchini litakalofanyika tarehe 8 Mwezi ujao katika jiji la Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja katika mtandao wa www.ar.co.tz bure kabisa ambapo atazindua rasmi kazi zake mpya za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanaume na wanawake.
Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Rehmtullah alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati zake za kuinua kiwango cha kazi za mitindo ndani ya nchi.
“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini ili kazi za wanamtindo na wabunifu wa mavazi hapa nchini ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Rehmtullah alisema kwamba onyesho hilo litakuwa la kipekee kwa sababu mavazi na onyesho litapambwa na rangi nyeupe,ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Alisema onyesho hilo ambalo litafanyika katika hoteli ya Serena litapambwa na wasanii mbalimbali wa muziki na wacheza shoo toka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Rehmtullah alisema onyesho hilo itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye binafsi kuonyesha muonekano mpya wa tasnia ya mitindo hapa nchini na nje ya nchini ili kuonyesha ni kwa jinsi ngani wanamitindo wa kitanzania wanavyoweza kuonyesha kazi zao.
Alisema kuwa tasnia ya mitindo kwa ujumla ina nafasi ya kipekee kwa wanamtindo chipukizi hapa nchini kujitokeza na kuonyesha kazi zao kwa watu mbalimbali hasa washika dau katika sekta hiyo.
‘kazi za mitindo na mavazi ndio mkombozi wa kweli katika kupunguza tatizo la ajira nchini Tanzania kwa sababu ni sekta inayokua kwa kasi kubwa na inatoa ajira kwa vijana wengi wa kike na kiume,’aliongeza
Onyesho hilo linategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 wakiwemo viongozi mbalimbali kama mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa mashirika mbalimbali.
Onyesho hilo litakuwa ni la mialiko maalum na limepewa jina la Ally Rehmtullah 2013 collection.
Wadhamini wa onyesho hilo ni Mercedez Benz, Belvedere Vodka, DULUX, RAHA, HUGO DOMINGO,THE Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Mo Blog, Quality Furniture na Mx Carter



KINDOILE AJITOSA UONGOZI KRFA

Ally Kindoile (Kulia) akiwa kwenye moja ya harakati zake za kuinua michezo, pichani wakati akiwa Mjumbe wa  Kamati ya Utendaji wa Villa Squad.
Na blogger team
 
MDAU wa michezo na aliewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Villa Squad Fc ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Ally Kindoile amejitosa kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), unaotarajiwa kufanyika mkoani humo Agosti 28 mwaka huu.

Akizungumza na gazeti la kila siku la Tanzania Daima, kwa njia ya simu jana, Kindoile ambaye pia aliwahi kukaimu kwa muda nafasi Mwenyekiti wa Villa kabla ya kushuka daraja, alisema kuwa, amechukua uamuzi wa kuwania nafasi hiyo, ili kuinua soka la Mkoa wa Kilimanjaro na pia kurudisha sifa na heshima iliyokuwepo miaka ya nyuma kwenye mchezo huo.
Kindoile, alibainisha mipango yake mikubwa kuwa ni pamoja na kupandisha timu ligi kuu na kunyakua mataji mbalimbali ikiwamo Taifa Cup.

“Naomba wadau wa michezo mkoani hapa, kwa pamoja kushirikiana kwa hali na nguvu ili kuleta maendeleo ya soka, kwa kuwa pamoja tukishirikiana tunayo nafasi ya kurudisha hali na morali kwa vijana na wanamichezo ndani ya Kilimanjaro na siku za usoni tupate timu yetu itakayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara,” alisema Kindoile.

Licha ya kuwa mdau wa michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Simba B na Idrisa Fc, kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya Kilimanjaro Rangers ya mkoani Kilimanjaro na amekuwa kwenye mstari wa mbele katika kusaidia vijana kwenye soka, huku kwa vipindi tofauti alifanikiwa kuipandisha timu ya Villa Ligi Kuu kwa vipindi viwili ikiwemo msimu 2010-2012.
 
 
 
 

Thursday, August 2, 2012

WAZEE WASTAAFU WAMTAKA PINDA KUSIKILIZAMADAI YAO



Mzee Mafita (kulia) akiwa na boga leke( kushoto) ni Andrew Chale,Mkurugenzi wa Habarimotomototz  Inc.
Mzee Mafita na wenzake zaidi ya 8,000 ambao ni wastaafu wanadai mkuongezewa Pensheni zao kutoka elf 50, na pia wapewe penshi hizo kwa wakati.

Na Blogger team

WAZEE wastaafu  Serikalini wamemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusikiliza kilio chao cha muda mrefu ikiwemo cha kuwaongezea pensheni zao na kuwapatia kwa wakati.

Akizungumza  mapema leo jijini Dar es Salaam, mmoja wa wazee hao James Mafita Mkazi wa Dar es Saalam, ambaye alikua mfanyakazi wa wizara ya kazi na ustawi wa jamii wakati huo, alisema kuwa zaidi ya wazee 8,000 ambao wanapata pensheni kutoka wizara ya Fedha, wamekua wakicheleweshewa kuingizwa fedha hizo licha ya kua ni kidogo.

“Mwaka, juzi, wakati wa kilele cha siku ya wazee Duniani, Oktoba Mosi, tuliweza muomba waziri mkuu atuongezee pensheni na tupate kwa wakati, lakini tunaona kimya maana kiasi cha 50,000 kwa wazee ambao hatuna kazi ni unyonyaji” alisema Mafita.

Mafita aliongeza kuwa licha  ya kuendelea kuomba ongezeko lao hilo la pensheni kwa Waziri mkuu, waliweza kuwakilisha tena kwenye kilele cha wazee mwaka jana iliyofanyika Mkoani, Lindi lakini bado hawajasilikilizwa.

“Sie wazee tumewezesha nchi hii kwa kuitumikia, lakini wameshindwa kutujali wengine tunafanya kazi kuuza maboga mitaani, lakini wao wanajipatia malupulupu umengi na kushindwa kutukumbuka” alisema Madita.

Mbali na hilo, aliomba wazira ya Fedha kuwapatia pensheni zao hizo kwa wakati kwani utaratibu uliopo sasa wanawacheleweshea kwa kuwapatia zaidi ya miezi minne tofauti na awali walikua wakiwapa kwa wakati na kumtaka Pinda asikie kilio chao haraka kabla ya kuanza utaratibu mwingine kama wafanyavyo wazee wanaodai haki zao hapa nchini.

Thursday, July 26, 2012

TAMASHA LA “CHAGGA DAY CULTURAL FESTIVAL 2012”

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga (Kulia) akielezea juu ya tamasha maalum la siku ya Wachaga  lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika siku ya Jumamosi Julai 28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo pia litasindikizwa na bendi za Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi vingine vya ngoma ya asili, (Kushoto) Ni Fredrick Mtaki, Afisamahusiano wa kampuni hiyo. (Picha na Andrew Chale).


Na Andrew Chale
Blogger Team.

BENDI  zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.

Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.

“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga

Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali

Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.

Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa  tamaduni zao  yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.

Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro,  SBC Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata Decorations.

Monday, July 23, 2012

NYOTA WA NOLLYWOOD;EBUBE NWAGBO

"Sina aibu nikiwa katika kazi"


LAGOS, Nigeria

JINA la mwigizaji Ebube Nwagbo limekuwa maarufu nchini Nigeria kwani ni mmoja kati ya wanadada waliofanikiwa kiusanii ikiwa ni pamoja na kutajwa kuwa mwenye mvuto wa hali ya juu katika Nollywood.
Kufanikiwa kwa mwanadada huyo kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wake ambao umemuwezesha kuzindua nywele zake za bandia alizozipatia jina la ‘Posh hair’ zikiwa zinauzika zaidi kwa watu wa kawaida wa nchini Nigeria.
Mwigizaji huyu kutoka Enugu, amezaliwa katika jimbo la Anambra.
Katika makala hii, mwanadada huyo anazungumzia historia ya maisha yake katika filamu na ya kawaida.

SWALI: Ni kazi gani kwa sasa unaitengeneza?
JIBU: Kwa sasa nipo katika upigaji wa picha za filamu yangu inayotayarishwa na Kampuni ya Get Rich Productions, lakini bado hatujaipatia jina, na nimecheza kama binti mdogo ambaye nilijiunga na kazi ya umalaya kwa ajili ya kusaidia maisha ya mama yangu. Filamu hiyo imewashirikisha wasanii kama vile Sam Dede, Atus kutoka Ghana, Ngozi Ezeonu na waigizaji wengine wa Nollywood.

SWALI: Ni kazi ngapi nyingine ulizotengeneza baada ya mwaka juzi kutangaza kupumzika uigizaji?
JIBU: Nimefanya kazi kibao kwa mwaka jana, na nyingi bado sijazitoa. Ninachokumbuka ni kama filamu 10 zikiwamo zile nilizoshirikishwa. Nilipokuwa nimesema nilipumzika sikumaanisha kwamba sikuwa nacheza filamu kabisa, bali nilikuwa nacheza kwa kiasi na muda mwingine nilikuwa nikitumia kufanya shughuli nyingine. Najua kwamba sitaigiza katika maisha yangu yote. Ndiyo sababu kuna kitu nahitaji kukizindua hivi karibuni.

SWALI: Je, ni kazi gani uliyokuwa ukijihusisha nayo kwa wakati huo?
JIBU: Nilikuwa nikijihusisha na kutangaza aina ya nywele bandia zinazojulikana kama  ‘Posh Hair’. Na kwa sasa natarajia kuzindua kampuni yangu kwa ushirikiano na rafiki yangu. Na ninamshukuru Mungu kwa biashara yangu kwenda vizuri.

SWALI: Nini faida yako katika biashara zako?
JIBU: Kabla ya kujiingiza katika biashara, maisha yangu yalikuwa yakitegemea zaidi uigizaji. Lakini nilipopata biashara nimeweza kufanya mambo mengi sana baada ya kujiongezea kipato.

SWALI: Unadhani ilikugharimu kwa kutoonekana kwenye filamu wakati ulipokuwa katika biashara?
JIBU: Ndiyo, lakini ninamshukuru Mungu kwa kunirejesha tena na kupokelewa upya kwa kishindo.

SWALI: Ipi mipango yako katika uigizaji?
JIBU: Kama nilivyosema, sitarajii kuigiza milele kwa kuwa kazi hii inahitaji muda mwingi sana na ni ngumu, kwa sasa najiandaa kustaafu.

SWALI: Vipi, nimesikia kuwa unajihusisha pia na muziki wa injili?
JIBU: Muziki wa Injili kwangu nafanya kama mapenzi na wala si kwa kazi, na hilo limechangiwa na kuandikiwa mashairi na rafiki zangu. Pia nimeimba muziki huo ili nioneshe kwamba hata kuimba naweza.

SWALI: Ni filamu gani unayoipenda sana kati ya zile ulizotengeneza?
JIBU: Filamu ninayoipenda ni ‘Arrested By Love’ niliyoigiza na Jim Iyke, Pete Edochie na wengineo.

SWALI: Unaonesha unaaaibu sana, uliwezaje kucheza filamu?
JIBU: Sina aibu nikiwa katika kazi na nimekuwa nikifurahia kazi ninayokuwa naifanya.

SWALI: Iwapo utakuwa unahitaji kuolewa unadhani ni mume gani anakufaa?
JIBU: Mwanaume yeyote muelewa na anayekuja kwangu kwa ajili yangu na si kwa ajili ya umaarufu wangu, sijali uwezo wake hata asipokuwa tajiri. Mwanaume mzuri kwangu ni yule atakayekuwa tayari kufa kwa ajili yangu.

SWALI: Unachukuliaje suala la kuendesha gari kali aina ya Hummer Jeep?
JIBU: Sidhani kama ni mwigizaji wa kwanza kuendesha gari hilo, kwani kuna waigizaji wengi wanaoendesha aina hiyo ya gari. Wapo wengi tu, labda wengi washangae kwa sababu ya umri wangu mdogo.



Saturday, July 21, 2012

FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA KUFANYIKA MKESHA WA UHURU

Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Kinondoni wakiwa kwenye pozi.
Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Kinondoni wakiwa kwenye pozi.
Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Kinondoni wakiwa kwenye pozi.
Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Kinondoni wakiwa kwenye pozi.

Na Andrew Chale (Blogger Team).

Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012, zimepangwa kufanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru w Tanzania tarehe 8-12-2012.
Tunakaribisha watu binafsi na makampuni yenye uwezo na yanapenda kuwa mawakala wetu wa kuaandaa fainali za Mikoa na Kanda watume maombi yao katika emai yetu missutaliitanzania@gmail.com .
  au piga simu namba 0715 318 278 Mikoa na kanda ambazo nafasi zipo wazi ni Pwani, Kigoma, Tabora, Shinyanga, Geita, Shimiyu, Geita, Singida, Dodoma, Morogoro, Ruvuma, Njombe, Tanga, Rukwa, Mbeya, Zanzibar, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati,  
Kanda ya Kusini, Kanda ya Mashariki, Vyuo Vikuu Kusini,Vyuo Vikuu kaskazini,Vyuo Vikuu Kati,Vyuo Vikuu Ziwa, Vyuo Vikuu Mashariki, Vyuo Vikuu Nyanda za Juu Kusini na mikoa ya Lindi na Mtwara